11. Moabu amestarehe tangu ujana wake, naye ametulia juu ya sira zake, wala hakumiminwa kutoka chombo kimoja kutiwa chombo kingine, wala hakwenda kufungwa; kwa hiyo ladha yake anakaa nayo, wala harufu yake haikubadilika.
12. Basi, tazama, siku zinakuja, asema BWANA, ambazo nitampelekea wamiminao, nao watammimina, nao watamwaga vyote vilivyomo vyomboni mwake, na kuzivunja chupa zake vipande vipande.
13. Na Moabu ataona haya kwa ajili ya Kemoshi, kama nyumba ya Israeli ilivyoona haya kwa ajili ya Betheli, matumaini yao.
14. Mwasemaje ninyi, Sisi tu mashujaa, watu hodari wa vita.
15. Moabu ameharibika, na moshi wa miji yake umepanda; na vijana wake wateule wametelemka kwenda kuchinjwa, asema Mfalme, ambaye jina lake ni BWANA wa majeshi.
16. Msiba wa Moabu umefika karibu,Na mateso yake yanafanya haraka.
17. Ninyi nyote mnaomzunguka, mlilieni,Nanyi nyote mlijuao jina lake, semeni,Jinsi ilivyovunjika fimbo ya enzi,Fimbo ile iliyokuwa nzuri!
18. Ee binti ukaaye Diboni,Shuka toka utukufu wako, ukae katika kiu;Maana atekaye Moabu amepanda juu yako,Ameziharibu ngome zako.
19. Wewe ukaaye Aroeri,Simama kando ya njia upeleleze;Mwulize mwanamume akimbiaye na mwanamke atorokaye,Sema, Imetendeka nini?
20. Moabu ameaibishwa, kwa maana amevunjika;Pigeni yowe na kulia;Tangazeni habari hii katika Arnoni,Ya kuwa Moabu ameharibika.
21. Na hukumu imeifikilia nchi tambarare; juu ya Holoni, na juu ya Yasa, na juu ya Mefaathi;
22. na juu ya Diboni, na juu ya Nebo, na juu ya Beth-diblathaimu;