Yer. 47:5-7 Swahili Union Version (SUV)

5. Upaa umeupata Gaza;Ashkeloni umenyamazishwaMabaki ya bonde lao;Hata lini utajikata-kata?

6. Ee upanga wa BWANA,Siku ngapi zitapita kabla hujatulia?Ujitie katika ala yako;Pumzika, utulie.

7. Utawezaje kutulia,Ikiwa BWANA amekupa agizo?Juu ya Ashkeloni na juu ya pwani,Ndipo alipoyaamuru hayo.

Yer. 47