4. kwa sababu ya siku ijayo kuwaangamiza Wafilisti wote, kukatilia mbali kila msaidizi wa Tiro na Sidoni asaliaye; maana BWANA atawaharibu Wafilisti, mabaki ya kisiwa cha Kaftori.
5. Upaa umeupata Gaza;Ashkeloni umenyamazishwaMabaki ya bonde lao;Hata lini utajikata-kata?
6. Ee upanga wa BWANA,Siku ngapi zitapita kabla hujatulia?Ujitie katika ala yako;Pumzika, utulie.
7. Utawezaje kutulia,Ikiwa BWANA amekupa agizo?Juu ya Ashkeloni na juu ya pwani,Ndipo alipoyaamuru hayo.