4. Ikawa Sedekia, mfalme wa Yuda, na watu wote wa vita walipowaona, ndipo wakakimbia, wakatoka mjini usiku, kwa njia ya bustani ya mfalme, kwa lango lililokuwa kati ya zile kuta mbili; naye akatoka kwa njia ya Araba.
5. Lakini jeshi la Wakaldayo wakawafuatia, wakampata Sedekia katika nchi tambarare ya Yeriko; nao walipomkamata, wakamleta kwa Nebukadreza, mfalme wa Babeli, huko Ribla katika nchi ya Hamathi, naye akatoa hukumu juu yake.
6. Ndipo mfalme wa Babeli akawaua wana wa Sedekia huko Ribla mbele ya macho yake; pia mfalme wa Babeli akawaua wakuu wote wa Yuda.
7. Pamoja na hayo akampofusha macho Sedekia, akamfunga kwa pingu ili amchukue mpaka Babeli.
8. Nao Wakaldayo wakaiteketeza nyumba ya mfalme, na nyumba za watu kwa moto, wakazibomoa kuta za Yerusalemu.