22. Nanyi mtakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wenu.
23. Tazama, tufani ya BWANA, yaani, ghadhabu yake, imetokea tufani ya kudumu; itawaangukia waovu vichwani.
24. Hasira kali ya BWANA haitarudi, hata atakapokwisha kutenda, hata atakapokwisha kuyatimiza makusudi ya moyo wake; katika siku za mwisho mtayafahamu haya.