6. oeni wake, mkazae wana na binti; kawaozeni wake wana wenu, mkawaoze waume binti zenu, wazae wana na binti; mkaongezeke huko wala msipungue.
7. Kautakieni amani mji ule, ambao nimewafanya mchukuliwe mateka, mkauombee kwa BWANA; kwa maana katika amani yake mji huo ninyi mtapata amani.
8. Maana BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Manabii walio kati yenu, na wabashiri wenu, wasiwadanganye ninyi, wala msisikilize ndoto zenu, mnazootesha.
9. Kwa maana kwa jina langu hutabiri maneno ya uongo kwenu; mimi sikuwatuma, asema BWANA.
10. Maana BWANA asema hivi, Babeli utakapotimiziwa miaka sabini, nitawajilia ninyi, na kulitimiza neno langu jema kwenu, kwa kuwarudisha mahali hapa.
11. Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema BWANA, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho.
12. Nanyi mtaniita, mtakwenda na kuniomba, nami nitawasikiliza.
13. Nanyi mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote.