Yer. 29:27-32 Swahili Union Version (SUV)

27. Mbona, basi, hukumkemea Yeremia wa Anathothi, ajifanyaye kuwa nabii kwenu,

28. ambaye ametuma watu kwetu katika Babeli, kusema, Uhamisho huu ni wa siku nyingi; jengeni nyumba, mkakae ndani yake; pandeni bustani, mkale matunda yake.

29. Na Sefania, kuhani, akasoma barua hii masikioni mwa Yeremia nabii.

30. Ndipo neno la BWANA likamjia Yeremia, kusema,

31. Uwapelekee habari watu wote waliohamishwa, kusema, BWANA asema hivi, katika habari za Shemaya, Mnehelami; Kwa sababu Shemaya amewatabiria ninyi, lakini sikumtuma mimi, naye amewatumainisha neno la uongo;

32. basi, BWANA asema hivi, Tazama, nitamwadhibu Shemaya, Mnehelami, na wazao wake; hatakuwa na mtu atakayekaa katika watu hawa, wala hatayaona mema nitakayowatendea watu wangu, asema BWANA; kwa sababu amenena maneno ya uasi juu ya BWANA.

Yer. 29