20. ambavyo Nebukadreza, mfalme wa Babeli, hakuvichukua, hapo alipomchukua Yekonia, mwana wa Yehoyakimu, mfalme wa Yuda, toka Yerusalemu mpaka Babeli, pamoja na wakuu wote wa Yuda, na Yerusalemu;
21. naam, BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, katika habari za vyombo vilivyobaki katika nyumba ya BWANA, na katika nyumba ya mfalme wa Yuda, na hapa Yerusalemu;
22. Vitachukuliwa mpaka Babeli, navyo vitakaa huko, hata siku ile nitakapovijilia, asema BWANA; hapo ndipo nitakapovileta tena, na kuvirudisha mahali hapa.