16. Pia nalisema na makuhani, na watu wote, nikisema, BWANA asema hivi, Msisikilize maneno ya manabii wenu, wanaowatabiria, wakisema, Tazameni, vyombo vya nyumba ya BWANA, baada ya muda kidogo, vitaletwa tena toka Babeli; maana wanawatabiria uongo.
17. Msiwasikilize; mtumikieni mfalme wa Babeli, mkaishi; kwani mji huu kufanywa ukiwa?
18. Lakini ikiwa hao ni manabii, na ikiwa neno la BWANA liko kwao, basi na wamwombe BWANA wa majeshi, kwamba vyombo vile vilivyosalia katika nyumba ya BWANA, na katika nyumba ya mfalme wa Yuda, na hapa Yerusalemu, visiende Babeli.
19. Maana BWANA wa majeshi asema hivi, katika habari za nguzo, na katika habari za bahari, na katika habari za matako yake, na katika habari za mabaki ya vyombo vilivyoachwa katika mji huu,