Maana atakuwa kama mti uliopandwa kando ya maji,Uenezao mizizi yake karibu na mto;Hautaona hofu wakati wa hari ujapo,Bali jani lake litakuwa bichi;Wala hautahangaika mwaka wa uchache wa mvua,Wala hautaacha kuzaa matunda.