Yer. 14:2-8 Swahili Union Version (SUV)

2. Yuda huomboleza,Na malango yake yamelegea;Wameketi chini wamevaa kaniki;Na kilio cha Yerusalemu kimepaa juu.

3. Na wakuu wao huwatuma watoto wao kwenye maji;Nao hufika visimani wasione maji;Hurudi, na vyombo vyao ni vitupu;Wametahayarika na kufadhaika,Na kuvifunika vichwa vyao.

4. Kwa sababu ya nchi iliyopasuka,Kwa kuwa mvua haikunyesha katika nchi,Wenye kulima wametahayarika,Na kuvifunika vichwa vyao.

5. Naam, kulungu naye uwandani amezaa,Akamwacha mwanawe kwa kuwa hapana majani.

6. Na punda-mwitu husimama juu ya vilele vya milima,Hutwetea pumzi kama mbwa-mwitu;Macho yao hayaoni sawasawa,Kwa kuwa hapana majani.

7. Ijapokuwa maovu yetu yanatushuhudia, lakini utende wewe kwa ajili ya jina lako, Ee BWANA, maana kurudi nyuma kwetu ni kwingi; tumekutenda dhambi.

8. Wewe uliye tumaini la Israeli, wewe uliye Mwokozi wake wakati wa taabu, kwa nini wewe umekuwa kama mtu akaaye katika nchi, hali ya mgeni, na kama mtu mwenye kusafiri, ageukaye upande ili kukaa usiku mmoja tu?

Yer. 14