8. Urithi wangu umekuwa kwangu kama simba msituni; ameinua sauti yake juu yangu; kwa sababu hiyo nimemchukia.
9. Je! Urithi wangu umekuwa kwangu kama ndege mwenye madoadoa? Ndege wakali wanamtulia pande zote? Enendeni, wakusanyeni pamoja wanyama wote wa mwituni, waleteni ili wale.
10. Wachungaji wengi wameliharibu shamba langu la mizabibu, wamelikanyaga fungu langu chini ya miguu yao, wamefanya fungu langu zuri kuwa jangwa la ukiwa.
11. Wamelifanya kuwa ukiwa, na kwa kuwa ni ukiwa linanililia; nchi yote imefanywa kuwa ukiwa, kwa sababu hapana mtu aliyeweka haya moyoni mwake.