14. BWANA asema hivi juu ya jirani zangu wote walio wabaya, waugusao urithi wangu niliowarithisha watu wangu Israeli, Tazama, nitawang’oa katika nchi yao, nami nitaing’oa nyumba ya Yuda isiwe kati yao.
15. Tena itakuwa, baada ya kuwang’oa, nitarudi na kuwahurumia; nami nitawaleta tena, kila mtu aingie katika urithi wake, na kila mtu aingie katika nchi yake.
16. Kisha itakuwa, ikiwa watajifunza kwa bidii njia za watu wangu, kuapa kwa jina langu, Kama BWANA aishivyo, vile vile kama walivyowafundisha watu wangu kuapa kwa Baali, ndipo watakapojengwa kati ya watu wangu.
17. Bali, kama hawataki kusikia, kung’oa nitaling’oa taifa lile, na kuliangamiza kabisa, asema BWANA.