Yer. 10:21-25 Swahili Union Version (SUV)

21. Kwa sababu wachungaji wamekuwa kama wanyama, wala hawakuuliza kwa BWANA; basi hawakufanikiwa, na makundi yao yote yametawanyika.

22. Sauti imesikiwa, Tazama, inakuja; mshindo mkuu kutoka nchi ya kaskazini, ili kuifanya miji ya Yuda kuwa ukiwa, makao ya mbweha.

23. Ee BWANA, najua ya kuwa njia ya mwanadamu haimo katika nafsi yake; kuelekeza hatua zake si katika uwezo wa mwanadamu.

24. Ee BWANA, unirudi kwa haki; si kwa hasira yako, usije ukaniangamiza.

25. Hasira yako uwamwagie mataifa wasiokujua, na jamaa zao wasioliitia jina lako; kwa maana wamemla Yakobo, naam, wamemla kabisa na kumwangamiza, na kuyafanya makao yake kuwa ukiwa.

Yer. 10