Yak. 1:3-10 Swahili Union Version (SUV)

3. mkifahamu ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huleta saburi.

4. Saburi na iwe na kazi kamilifu, mpate kuwa wakamilifu na watimilifu bila kupungukiwa na neno.

5. Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa.

6. Ila na aombe kwa imani, pasipo shaka yo yote; maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari lililochukuliwa na upepo, na kupeperushwa huku na huku.

7. Maana mtu kama yule asidhani ya kuwa atapokea kitu kwa Bwana.

8. Mtu wa nia mbili husita-sita katika njia zake zote.

9. Lakini ndugu asiye na cheo na afurahi kwa kuwa ametukuzwa;

10. bali tajiri kwa kuwa ameshushwa; kwa maana kama ua la majani atatoweka.

Yak. 1