Wim. 7:1-7 Swahili Union Version (SUV)

1. Siti msharifu, jinsi zilivyo nzuriHatua zako katika mitalawanda.Mapaja yako ya mviringo ni kama johari,Kazi ya mikono ya fundi mstadi;

2. Kitovu chako ni kama bilauri iliyoviringana,Na isikose divai iliyochanganyika;Tumbo lako ni mfano wa chungu ya ngano,Iliyozungukwa na ugo wa nyinyoro;

3. Maziwa yako mawili ni kama wana-paa wawili,Ambao ni mapacha ya paa;

4. Shingo yako ni kama huo mnara wa pembe;Macho yako kama viziwa vya Heshboni,Karibu na mlango wa Beth-rabi;Pua yako ni kama mnara wa Lebanoni,Unaoelekea Dameski;

5. Kichwa chako juu yako ni kama Karmeli,Na nywele za kichwa chako kama urujuani,Mfalme amenaswa na mashungu yake.

6. Jinsi yalivyo mazuri, yalivyo matamu,Mapenzi katikati ya anasa!

7. Kimo chako kimefanana na mtende,Na maziwa yako na vichala.

Wim. 7