6. Meno yako kama kundi la kondoo,Wakipanda kutoka kuoshwa;Ambao kila mmoja amezaa mapacha,Wala hakuna aliyefiwa kati yao.
7. Mashavu yako ni kama kipande cha komamanga,Nyuma ya barakoa yako.
8. Wako malkia sitini, na masuria themanini,Na wanawali wasiohesabika;
9. Hua wangu, mkamilifu wangu, ni mmoja tu,Mtoto wa pekee wa mamaye.Ndiye kipenzi chake aliyemzaa,Binti wakamwona wakamwita heri;Malkia na masuria nao wakamwona,Wakamsifu, wakisema,