1. Mimi ni ua la uwandani,Ni nyinyoro ya mabondeni.
2. Kama nyinyoro kati ya miiba,Kadhalika mpenzi wangu kati ya binti.
3. Kama mpera kati ya miti ya msituni,Kadhalika mpendwa wangu kati ya vijana.Naliketi kivulini mwake kwa furaha,Na matunda yake naliyaonja kuwa matamu.
4. Akanileta mpaka nyumba ya karamu,Na bendera yake juu yangu ni mapenzi.
5. Nishibisheni zabibu, niburudisheni kwa mapera,Kwa maana nimezimia kwa mapenzi.
6. Mkono wake wa kushoto uko chini ya kichwa changu,Nao wa kuume unanikumbatia!
7. Nawasihi, enyi binti za Yerusalemu,Kwa paa na kwa ayala wa porini,Msiyachochee mapenzi, wala kuyaamsha,Hata yatakapoona vema yenyewe.