3. akisema, Msiidhuru nchi, wala bahari, wala miti, hata tutakapokwisha kuwatia muhuri watumwa wa Mungu wetu juu ya vipaji vya nyuso zao.
4. Nikasikia hesabu yao waliotiwa muhuri katika kila kabila ya Waisraeli, watu mia na arobaini na nne elfu.
5. Wa kabila ya Yuda kumi na mbili elfu waliotiwa muhuri.Wa kabila ya Reubeni kumi na mbili elfu.Wa kabila ya Gadi kumi na mbili elfu.
6. Wa kabila ya Asheri kumi na mbili elfu.Wa kabila ya Naftali kumi na mbili elfu.Wa kabila ya Manase kumi na mbili elfu.
7. Wa kabila ya Simeoni kumi na mbili elfu.Wa kabila ya Lawi kumi na mbili elfu.Wa kabila ya Isakari kumi na mbili elfu.