Ufu. 3:6-8 Swahili Union Version (SUV)

6. Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa.

7. Na kwa malaika wa kanisa lililoko Filadelfia andika;Haya ndiyo anenayo yeye aliye mtakatifu, aliye wa kweli, aliye na ufunguo wa Daudi, yeye mwenye kufungua wala hapana afungaye, naye afunga wala hapana afunguaye.

8. Nayajua matendo yako. Tazama, nimekupa mlango uliofunguliwa mbele yako, ambao hapana awezaye kuufunga, kwa kuwa unazo nguvu kidogo, nawe umelitunza neno langu, wala hukulikana jina langu.

Ufu. 3