16. Basi Naomi akamtwaa yule mtoto, akamweka kifuani pake, akawa mlezi wake.
17. Nao wale wanawake waliokuwa jirani zake wakampa jina, wakisema, Naomi amezaliwa mwana; wakamwita jina lake Obedi; yeye ndiye baba yake Yese, aliye baba yake Daudi.
18. Hivi ndivyo vizazi vya Peresi; Peresi alimzaa Hesroni;
19. na Hesroni akamzaa Ramu; na Ramu akamzaa Aminadabu;
20. na Aminadabu akamzaa Nashoni; na Nashoni akamzaa Salmoni;
21. na Salmoni akamzaa Boazi; na Boazi akamzaa Obedi;