16. Naye Ruthu akasema,Usinisihi nikuache,Nirejee nisifuatane nawe;Maana wewe uendako nitakwenda,Na wewe ukaapo nitakaa.Watu wako watakuwa watu wangu,Na Mungu wako atakuwa Mungu wangu;
17. Pale utakapokufa nitakufa nami,Na papo hapo nitazikwa;BWANA anitende vivyo na kuzidi,Ila kufa tu kutatutenga wewe nami.
18. Basi alipomwona kuwa amekaza nia yake kufuatana naye, aliacha kusema naye.
19. Hivyo hao wakaendelea wote wawili hata walipofika Bethlehemu. Na ikawa walipofika Bethlehemu, mji wote ulitaharuki kwa habari zao. Nao wanawake wakasema, Je! Huyu ni Naomi?
20. Akawaambia, Msiniite Naomi, niiteni Mara, kwa sababu Mwenyezi Mungu amenitenda mambo machungu sana.
21. Mimi nalitoka hali nimejaa, naye BWANA amenirudisha sina kitu, kwani kuniita Naomi, ikiwa BWANA ameshuhudia juu yangu, na Mwenyezi Mungu amenitesa?
22. Basi Naomi akarudi; pamoja na Ruthu Mmoabi, mkwewe; ambao walirudi kutoka nchi ya Moabu; nao wakafika Bethlehemu mwanzo wa mavuno ya shayiri.