4. Hasha! Mungu aonekane kuwa amini na kila mtu mwongo; kama ilivyoandikwa,Ili ujulike kuwa una haki katika maneno yako,Ukashinde uingiapo katika hukumu.
5. Lakini, ikiwa udhalimu wetu waithibitisha haki ya Mungu, tuseme nini? Je! Mungu ni dhalimu aletaye ghadhabu? (Nasema kwa jinsi ya kibinadamu.)
6. Hasha! Kwa maana hapo Mungu atawezaje kuuhukumu ulimwengu?
7. Lakini, ikiwa kweli ya Mungu imezidi kudhihirisha utukufu wake kwa sababu ya uongo wangu, mbona mimi ningali nahukumiwa kuwa ni mwenye dhambi?
8. Kwa nini tusiseme (kama tulivyosingiziwa, na kama wengine wanavyokaza kusema ya kwamba twasema hivyo), Na tufanye mabaya, ili yaje mema? Ambao kuhukumiwa kwao kuna haki.
9. Ni nini basi? Tu bora kuliko wengine? La! Hata kidogo. Kwa maana tumekwisha kuwashitaki Wayahudi na Wayunani ya kwamba pia wamekuwa chini ya dhambi;
10. kama ilivyoandikwa, ya kwamba,Hakuna mwenye haki hata mmoja.
11. Hakuna afahamuye;Hakuna amtafutaye Mungu.
12. Wote wamepotoka, wameoza wote pia;Hakuna mtenda mema, la! Hata mmoja.
13. Koo lao ni kaburi wazi,Kwa ndimi zao wametumia hila.Sumu ya fira i chini ya midomo yao.
14. Vinywa vyao vimejaa laana na uchungu.
15. Miguu yao ina mbio kumwaga damu.
16. Uharibifu na mashaka yamo njiani mwao.
17. Wala njia ya amani hawakuijua.
18. Kumcha Mungu hakupo machoni pao.