Rum. 3:1-6 Swahili Union Version (SUV)

1. Basi Myahudi ana ziada gani? Na kutahiriwa kwafaa nini?

2. Kwafaa sana kwa kila njia. Kwanza kwa kuwa wamekabidhiwa mausia ya Mungu.

3. Ni nini, basi, ikiwa baadhi yao hawakuamini? Je! Kutokuamini kwao kutaubatili uaminifu wa Mungu?

4. Hasha! Mungu aonekane kuwa amini na kila mtu mwongo; kama ilivyoandikwa,Ili ujulike kuwa una haki katika maneno yako,Ukashinde uingiapo katika hukumu.

5. Lakini, ikiwa udhalimu wetu waithibitisha haki ya Mungu, tuseme nini? Je! Mungu ni dhalimu aletaye ghadhabu? (Nasema kwa jinsi ya kibinadamu.)

6. Hasha! Kwa maana hapo Mungu atawezaje kuuhukumu ulimwengu?

Rum. 3