4. Kwa kuwa kama vile katika mwili mmoja tuna viungo vingi, wala viungo vyote havitendi kazi moja;
5. Vivyo hivyo na sisi tulio wengi tu mwili mmoja katika Kristo, na viungo, kila mmoja kwa mwenzake.
6. Basi kwa kuwa tuna karama zilizo mbalimbali, kwa kadiri ya neema mliyopewa; ikiwa unabii, tutoe unabii kwa kadiri ya imani;
7. ikiwa huduma, tuwemo katika huduma yetu; mwenye kufundisha, katika kufundisha kwake;
8. mwenye kuonya, katika kuonya kwake; mwenye kukirimu, kwa moyo mweupe; mwenye kusimamia kwa bidii mwenye kurehemu, kwa furaha.
9. Pendo na lisiwe na unafiki lichukieni lililo ovu, mkiambatana na lililo jema.
10. Kwa pendo la udugu, mpendane ninyi kwa ninyi; kwa heshima mkiwatanguliza wenzenu;
11. kwa bidii, si walegevu; mkiwa na juhudi katika roho zenu; mkimtumikia Bwana;
12. kwa tumaini, mkifurahi; katika dhiki, mkisubiri; katika kusali, mkidumu;
13. kwa mahitaji ya watakatifu, mkifuata ukarimu; katika kukaribisha wageni mkijitahidi.
14. Wabarikini wanaowaudhi; barikini, wala msilaani.
15. Furahini pamoja nao wafurahio; lieni pamoja nao waliao.