Rum. 12:12-20 Swahili Union Version (SUV)

12. kwa tumaini, mkifurahi; katika dhiki, mkisubiri; katika kusali, mkidumu;

13. kwa mahitaji ya watakatifu, mkifuata ukarimu; katika kukaribisha wageni mkijitahidi.

14. Wabarikini wanaowaudhi; barikini, wala msilaani.

15. Furahini pamoja nao wafurahio; lieni pamoja nao waliao.

16. Mpatane nia zenu ninyi kwa ninyi. Msinie yaliyo makuu, lakini mkubali kushughulishwa na mambo manyonge. Msiwe watu wa kujivunia akili.

17. Msimlipe mtu ovu kwa ovu. Angalieni yaliyo mema machoni pa watu wote.

18. Kama yamkini, kwa upande wenu, mkae katika amani na watu wote.

19. Wapenzi, msijilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu; maana imeandikwa, Kisasi ni juu yangu mimi; mimi nitalipa, anena Bwana.

20. Lakini, Adui yako akiwa na njaa, mlishe; akiwa na kiu, mnyweshe; maana ufanyapo hivyo, utampalia makaa ya moto kichwani pake.

Rum. 12