Rum. 11:28-34 Swahili Union Version (SUV)

28. Basi kwa habari ya Injili wamekuwa adui kwa ajili yenu; bali kwa habari ya kule kuchaguliwa wamekuwa wapenzi kwa ajili ya baba zetu.

29. Kwa sababu karama za Mungu hazina majuto, wala mwito wake.

30. Kwa maana kama ninyi zamani mlivyomwasi Mungu, lakini sasa mmepata rehema kwa kuasi kwao;

31. kadhalika na hao wameasi sasa, ili kwa kupata rehema kwenu wao nao wapate rehema.

32. Maana Mungu amewafunga wote pamoja katika kuasi ili awarehemu wote.

33. Jinsi zilivyo kuu utajiri na hekima na maarifa ya Mungu! Hukumu zake hazichunguziki, wala njia zake hazitafutikani!

34. Maana ni nani aliyeijua nia ya Bwana? Au ni nani aliyekuwa mshauri wake?

Rum. 11