Rum. 10:12-14 Swahili Union Version (SUV)

12. Kwa maana hakuna tofauti ya Myahudi na Myunani; maana yeye yule ni Bwana wa wote, mwenye utajiri kwa wote wamwitao;

13. kwa kuwa, Kila atakayeliitia Jina la Bwana ataokoka.

14. Basi wamwiteje yeye wasiyemwamini? Tena wamwaminije yeye wasiyemsikia? Tena wamsikieje pasipo mhubiri?

Rum. 10