17. Macho yetu yamechokaKwa kuutazamia bure msaada wetu;Katika kungoja kwetu tumengojea taifaLisiloweza kutuokoa.
18. Wanatuvizia hatua zetu,Hata hatuwezi kwenda katika njia zetu;Mwisho wetu umekaribia, siku zetu zimetimia;Maana mwisho wetu umefika.
19. Waliotufuatia ni wepesiKuliko tai za mbinguni;Hao walitufuatia milimani,Nao walituotea jangwani.
20. Pumzi ya mianzi ya pua zetu, masihi wa BWANA,Alikamatwa katika marima yao;Ambaye kwa habari zake tulisema,Chini ya kivuli chake tutakaa kati ya mataifa.
21. Furahi, ushangilie, Ee binti Edomu,Ukaaye katika nchi ya Usi;Hata kwako kikombe kitapita,Utalewa, na kujifanya uchi.
22. Uovu wako umetimia, Ee binti Sayuni;Hatakuhamisha tena;Atapatiliza uovu wako, Ee binti Edomu;Atazivumbua dhambi zako.