Omb. 4:11-18 Swahili Union Version (SUV)

11. BWANA ameitimiza kani yake,Ameimimina hasira yake kali;Naye amewasha moto katika SayuniUlioiteketeza misingi yake.

12. Wafalme wa dunia hawakusadiki,Wala wote wakaao duniani,Ya kwamba mtesi na adui wangeingiaKatika malango ya Yerusalemu.

13. Ni kwa sababu ya dhambi za manabii wakeNa maovu ya makuhani wake,Walioimwaga damu ya wenye hakiKatikati yake.

14. Hutanga-tanga njiani kama vipofu,Wametiwa unajisi kwa damu;Hata ikawa watu wasiwezeKuyagusa mavazi yao.

15. Watu waliwapigia kelele, Ondokeni, Uchafu,Ondokeni, ondokeni, msiguse;Walipokimbia na kutanga-tanga, watu walisema kati ya mataifa,Hawatakaa hapa tena.

16. Hasira ya BWANA imewatenga,Yeye hatawaangalia tena;Hawakujali nafsi za wale makuhani,Hawakuwaheshimu wazee wao.

17. Macho yetu yamechokaKwa kuutazamia bure msaada wetu;Katika kungoja kwetu tumengojea taifaLisiloweza kutuokoa.

18. Wanatuvizia hatua zetu,Hata hatuwezi kwenda katika njia zetu;Mwisho wetu umekaribia, siku zetu zimetimia;Maana mwisho wetu umefika.

Omb. 4