8. Naam, nikilia na kuomba msaada,Huyapinga maombi yangu.
9. Ameziziba njia zangu kwa mawe yaliyochongwa;Ameyapotosha mapito yangu.
10. Alivyo kwangu ni kama dubu aoteaye,Kama simba aliye mafichoni.
11. Amezigeuza njia zangu, na kunirarua-rarua;Amenifanya ukiwa.
12. Ameupinda upinde wake,Na kunifanya niwe shabaha kwa mshale.
13. Amenichoma viunoKwa mishale ya podo lake.
14. Nimekuwa dhihaka kwa watu wangu wote;Wimbo wao mchana kutwa.
15. Amenijaza uchungu,Amenikinaisha kwa pakanga.
16. Amenivunja meno kwa changarawe;Amenifunika majivu.
17. Umeniweka nafsi yangu mbali na amani;Nikasahau kufanikiwa.
18. Nikasema, Nguvu zangu zimepotea,Na tumaini langu kwa BWANA.
19. Kumbuka mateso yangu, na msiba wangu,Pakanga na nyongo.
20. Nafsi yangu ikali ikiyakumbuka hayo,Nayo imeinama ndani yangu.