Omb. 3:52-60 Swahili Union Version (SUV)

52. Walio adui zangu bila sababuWameniwinda sana kama ndege;

53. Wameukatilia mbali uhai wangu gerezani,Na kutupa jiwe juu yangu.

54. Maji mengi yalipita juu ya kichwa changu,Nikasema, Nimekatiliwa mbali.

55. Naliliitia jina lako, BWANA, kutoka lile shimoLiendalo chini kabisa.

56. Ukaisikia sauti yangu; usifiche sikio lakoIli usisikie pumzi yangu, kwa kilio changu.

57. Ulinikaribia siku ile nilipokulilia;Ukasema, Usiogope.

58. Ee BWANA umenitetea mateto ya nafsi yangu;Umeukomboa uhai wangu.

59. Umekuona kudhulumiwa kwangu, Ee BWANA;Unihukumie neno langu.

60. Umekiona kisasi chao chote,Na mashauri yao yote juu yangu.

Omb. 3