41. Na tumwinulie Mungu aliye mbinguniMioyo yetu na mikono.
42. Sisi tumekosa na kuasi;Wewe hukusamehe.
43. Umetufunika kwa hasira na kutufuatia;Umeua, wala hukuona huruma.
44. Umejifunika nafsi yako kwa wingu,Maombi yetu yasipite.
45. Umetufanya kuwa takataka, na vifusiKatikati ya mataifa.
46. Juu yetu adui zetu woteWametupanulia vinywa vyao.
47. Hofu imetujilia na shimo,Ukiwa na uharibifu.
48. Jicho langu lachuruzika mito ya majiKwa ajili ya uvunjifu wa binti ya watu wangu.
49. Jicho langu latoka machozi lisikome,Wala haliachi;
50. Hata BWANA atakapoangaliaNa kutazama toka mbinguni.