Omb. 3:32-43 Swahili Union Version (SUV)

32. Maana ajapomhuzunisha atamrehemu,Kwa kadiri ya wingi wa huruma zake.

33. Maana moyo wake hapendi kuwatesa wanadamu.Wala kuwahuzunisha.

34. Kuwaseta chini kwa miguuWafungwa wote wa duniani,

35. Kuipotosha hukumu ya mtuMbele zake Aliye juu,

36. Na kumnyima mtu haki yake,Hayo Bwana hayaridhii kabisa.

37. Ni nani asemaye neno nalo likafanyika,Ikiwa Bwana hakuliagiza?

38. Je! Katika kinywa chake Aliye juuHayatoki maovu na mema?

39. Mbona anung’unika mwanadamu aliye haiMtu akiadhibiwa kwa dhambi zake?

40. Na tuchunguze njia zetu na kuzijaribu,Na kumrudia BWANA tena.

41. Na tumwinulie Mungu aliye mbinguniMioyo yetu na mikono.

42. Sisi tumekosa na kuasi;Wewe hukusamehe.

43. Umetufunika kwa hasira na kutufuatia;Umeua, wala hukuona huruma.

Omb. 3