25. BWANA ni mwema kwa hao wamngojeao,Kwa hiyo nafsi imtafutayo.
26. Ni vema mtu autarajie wokovu wa BWANANa kumngojea kwa utulivu.
27. Ni vema mwanadamu aichukue niraWakati wa ujana wake.
28. Na akae peke yake na kunyamaza kimya;Kwa sababu Bwana ameweka hayo juu yake.
29. Na atie kinywa chake mavumbini;Ikiwa yamkini liko tumaini.
30. Na amwelekezee yule ampigaye shavu lake;Ashibishwe mashutumu.
31. Kwa kuwa Bwana hatamtupa mtuHata milele.
32. Maana ajapomhuzunisha atamrehemu,Kwa kadiri ya wingi wa huruma zake.
33. Maana moyo wake hapendi kuwatesa wanadamu.Wala kuwahuzunisha.