20. Nafsi yangu ikali ikiyakumbuka hayo,Nayo imeinama ndani yangu.
21. Najikumbusha neno hili,Kwa hiyo nina matumaini.
22. Ni huruma za BWANA kwamba hatuangamii,Kwa kuwa rehema zake hazikomi.
23. Ni mpya kila siku asubuhi;Uaminifu wako ni mkuu.
24. BWANA ndiye fungu langu, husema nafsi yangu,Kwa hiyo nitamtumaini yeye.
25. BWANA ni mwema kwa hao wamngojeao,Kwa hiyo nafsi imtafutayo.
26. Ni vema mtu autarajie wokovu wa BWANANa kumngojea kwa utulivu.
27. Ni vema mwanadamu aichukue niraWakati wa ujana wake.
28. Na akae peke yake na kunyamaza kimya;Kwa sababu Bwana ameweka hayo juu yake.
29. Na atie kinywa chake mavumbini;Ikiwa yamkini liko tumaini.
30. Na amwelekezee yule ampigaye shavu lake;Ashibishwe mashutumu.
31. Kwa kuwa Bwana hatamtupa mtuHata milele.
32. Maana ajapomhuzunisha atamrehemu,Kwa kadiri ya wingi wa huruma zake.
33. Maana moyo wake hapendi kuwatesa wanadamu.Wala kuwahuzunisha.
34. Kuwaseta chini kwa miguuWafungwa wote wa duniani,
35. Kuipotosha hukumu ya mtuMbele zake Aliye juu,
36. Na kumnyima mtu haki yake,Hayo Bwana hayaridhii kabisa.
37. Ni nani asemaye neno nalo likafanyika,Ikiwa Bwana hakuliagiza?
38. Je! Katika kinywa chake Aliye juuHayatoki maovu na mema?
39. Mbona anung’unika mwanadamu aliye haiMtu akiadhibiwa kwa dhambi zake?
40. Na tuchunguze njia zetu na kuzijaribu,Na kumrudia BWANA tena.