Omb. 3:1-14 Swahili Union Version (SUV)

1. Mimi ni mtu aliyeona matesoKwa fimbo ya ghadhabu yake.

2. Ameniongoza na kuniendesha katika gizaWala si katika nuru.

3. Hakika juu yangu augeuza mkono wakeMara kwa mara mchana wote.

4. Amechakaza nyama yangu na ngozi yangu;Ameivunja mifupa yangu.

5. Amejenga boma juu yangu,Na kunizungusha uchungu na uchovu.

6. Amenikalisha penye giza,Kama watu waliokufa zamani.

7. Amenizinga pande zote hata siwezi kutoka;Ameufanya mnyororo wangu mzito.

8. Naam, nikilia na kuomba msaada,Huyapinga maombi yangu.

9. Ameziziba njia zangu kwa mawe yaliyochongwa;Ameyapotosha mapito yangu.

10. Alivyo kwangu ni kama dubu aoteaye,Kama simba aliye mafichoni.

11. Amezigeuza njia zangu, na kunirarua-rarua;Amenifanya ukiwa.

12. Ameupinda upinde wake,Na kunifanya niwe shabaha kwa mshale.

13. Amenichoma viunoKwa mishale ya podo lake.

14. Nimekuwa dhihaka kwa watu wangu wote;Wimbo wao mchana kutwa.

Omb. 3