16. Juu yako adui zako woteWamepanua vinywa vyao;Huzomea, husaga meno yao,Husema, Tumemmeza;Hakika siku hii ndiyo tuliyoitazamia;Tumeipata, tumeiona.
17. BWANA ameyatenda aliyoyakusudia; amelitimiza neno lake,Aliloliamuru siku za kale;Ameangusha hata chini,Wala hakuona huruma;Naye amemfurahisha adui juu yako,Ameitukuza pembe ya watesi wako.
18. Mioyo yao ilimlilia Bwana;Ee ukuta wa binti Sayuni!Machozi na yachuruzike kama mtoMchana na usiku;Usijipatie kupumzika;Mboni ya jicho lako isikome.
19. Inuka, ulalamike usiku,Mwanzo wa makesha yake;Mimina moyo wako kama maji usoni pa Bwana;Umwinulie mikono yako;Kwa uhai wa watoto wako wachanga wazimiao kwa njaa,Mwanzo wa kila njia kuu.