Neh. 7:66-70 Swahili Union Version (SUV)

66. Basi hilo kusanyiko lote zima, jumla yake ilikuwa watu arobaini na mbili elfu na mia tatu na sitini,

67. tena zaidi ya hao, kulikuwa na watumishi wao waume kwa wake, ambao walikuwa elfu saba na mia tatu na thelathini na saba; kisha walikuwa na waimbaji waume kwa wake mia mbili arobaini na watano.

68. Farasi zao walikuwa mia saba thelathini na sita; nyumbu zao, mia mbili arobaini na watano;

69. ngamia zao, mia nne thelathini na watano; punda zao, elfu sita na mia saba na ishirini.

70. Na baadhi ya wakuu wa mbari za mababa walitoa mali kwa ajili ya kazi hii. Yule Tirshatha akatoa kwa ajili ya hazina darkoni za dhahabu elfu moja, na mabakuli hamsini, na mavazi ya makuhani mia tano na thelathini.

Neh. 7