6. Shemaya, Yoyaribu, Yedaya;
7. Salu, Amoki, Hilkia, Yedaya. Hawa walikuwa wakuu wa makuhani na ndugu zao siku za Yoshua.
8. Tena Walawi; Yeshua, Binui, Kadmieli, Sherebia, Yuda, na Matania, aliyekuwa juu ya shukrani, yeye na ndugu zake.
9. Tena Bakbukia na Uno, ndugu zao, kuwaelekea kwa zamu.
10. Naye Yoshua akamzaa Yoyakimu, Yoyakimu akamzaa Eliashibu, Eliashibu akamzaa Yoyada,
11. Yoyada akamzaa Yohana, Yohana akamzaa Yadua.