Neh. 11:17-31 Swahili Union Version (SUV)

17. na Matania, mwana wa Mika, mwana wa Zikri, mwana wa Asafu, mkuu mwenye kuanzisha shukrani katika sala, na Bakbukia, wa pili wake miongoni mwa nduguze; na Obadia, mwana wa Shemaya, mwana wa Galali, mwana wa Yeduthuni.

18. Walawi wote waliokaa katika mji mtakatifu walikuwa watu mia mbili themanini na wanne.

19. Pamoja na hao, mabawabu; Akubu, Talmoni, na ndugu zao waliolinda malangoni, walikuwa watu mia na sabini na wawili.

20. Na Israeli waliosalia, katika hao makuhani, na Walawi, walikuwamo mijini mwote mwa Yuda, kila mtu katika milki yake.

21. Lakini Wanethini walikuwa wakikaa Ofeli; na juu ya Wanethini walikuwa Siha na Gishpa.

22. Naye msimamizi wa Walawi huko Yerusalemu, ni Uzi, mwana wa Bani, mwana wa Hashabia, mwana wa Matania, mwana wa Mika, wa wana wa Asafu, hao waimbaji, alikuwa juu ya kazi ya nyumba ya Mungu.

23. Kwa kuwa palikuwa na amri ya mfalme juu yao, na agizo la hakika walilowekewa waimbaji, kama ilivyohusika na kila siku.

24. Na Pethahia, mwana wa Meshezabeli, wa wana wa Zera, mwana wa Yuda, alikuwa wakili wa mfalme kwa habari ya mambo yote ya watu.

25. Na katika habari za vijiji na mashamba yake; wengine wa wana wa Yuda walikuwa wakikaa Kiriath-arba na vijiji vyake, na katika Diboni na vijiji vyake, na Yekabzeeli na vijiji vyake;

26. na katika Yeshua, na Molada, na Beth-peleti;

27. na Hazar-shuali, na Beer-sheba na vijiji vyake;

28. na katika Siklagi, na Mekona na vijiji vyake;

29. na katika Enrimoni, na Sora, na Yarmuthi;

30. Zanoa, Adulamu na vijiji vyake, Lakishi na mashamba yake, Azeka na vijiji vyake. Hivyo wakatua toka Beer-sheba mpaka bonde la Hinomu.

31. Wana wa Benyamini nao walikuwa wakikaa Geba, na Mikmashi, na Aiya, na Beth-eli na vijiji vyake;

Neh. 11