Neh. 11:13-18 Swahili Union Version (SUV)

13. na ndugu zake, wakuu wa mbari za mababa, watu mia mbili arobaini na wawili; na Maasai, mwana wa Azareli, mwana wa Azai, mwana wa Meshilemothi, mwana wa Imeri,

14. na ndugu zao, waume mashujaa, watu mia na ishirini na wanane; na msimamizi wao alikuwa Zabdieli, mmojawapo wa hao wakuu.

15. Na wa Walawi; Shemaya, mwana wa Hashubu, mwana wa Azrikamu, mwana wa Hashabia, mwana wa Buni;

16. na Shabethai na Yozabadi, wa wakuu wa Walawi, walioisimamia kazi ya nje ya nyumba ya Mungu;

17. na Matania, mwana wa Mika, mwana wa Zikri, mwana wa Asafu, mkuu mwenye kuanzisha shukrani katika sala, na Bakbukia, wa pili wake miongoni mwa nduguze; na Obadia, mwana wa Shemaya, mwana wa Galali, mwana wa Yeduthuni.

18. Walawi wote waliokaa katika mji mtakatifu walikuwa watu mia mbili themanini na wanne.

Neh. 11