5. Awakumbuka watu wake wenye heshima;Wanajikwaa katika mwendo wao;Wanafanya haraka waende ukutani;Nacho kitu cha kuwafunika kimewekwa tayari.
6. Malango ya mito yamefunguka, na jumba la mfalme limeyeyushwa.
7. Husabu naye amefunuliwa, anachukuliwa, na wajakazi wake wanalia kama kwa sauti ya hua, wakipiga-piga vifua vyao.
8. Lakini Ninawi tokea zamani amekuwa kama ziwa la maji; ila hata sasa wanakimbia; Simameni! Simameni! Lakini hapana hata mmoja atazamaye nyuma.
9. Chukueni nyara za fedha;Chukueni nyara za dhahabu;Kwa maana ni akiba isiyoisha,Fahari ya vyombo vipendezavyo.
10. Amekuwa utupu, na ukiwa, na uharibifu; hata moyo unayeyuka, na magoti yanagongana-gongana; viunoni mwote mna utungu, na nyuso za wote zimekuwa nyeupe kwa hofu.
11. Kao la simba li wapi? Na mahali walishapo wana-simba pa wapi, mahali walipotembea simba mume na simba mke na mwana-simba, wala hapana aliyewatia hofu?
12. Simba alirarua vipande vipande chakula cha kuwatosha watoto wake, aliwasongea wake zake nyama, aliyajaza mapango yake mateka, na makao yake aliyajaza mawindo.
13. Tazama, mimi ni juu yako, asema BWANA wa majeshi, nami nitayateketeza magari yako ya vita katika moshi, na upanga utawala wana-simba wako; nami nitayakatilia mbali mawindo yako katika nchi, na sauti za wajumbe wako hazitasikiwa tena kamwe.