Nah. 1:6-11 Swahili Union Version (SUV)

6. Ni nani awezaye kusimama mbele za ghadhabu yake, naye ni nani awezaye kukaa katika ukali wa hasira yake? Hasira yake kali humwagwa kama moto, nayo majabali yapasuliwa na yeye.

7. BWANA ni mwema, ni ngome siku ya taabu; naye huwajua hao wamkimbiliao.

8. Lakini kwa gharika ifurikayo atapakomesha kabisa mahali pake, na kuwafuatia adui zake hata gizani.

9. Mnawaza nini juu ya BWANA? Yeye atakomesha kabisa; mateso hayatainuka mara ya pili.

10. Kwa maana wangawa kama miiba iliyotatana, na kunyweshwa kana kwamba ni katika kunywa kwao, wataliwa kabisa kama mabua makavu.

11. Ametoka mmoja kwako, aniaye mabaya juu ya BWANA, atoaye mashauri yasiyofaa kitu.

Nah. 1