Nah. 1:11-15 Swahili Union Version (SUV)

11. Ametoka mmoja kwako, aniaye mabaya juu ya BWANA, atoaye mashauri yasiyofaa kitu.

12. BWANA asema hivi, Ijapokuwa wana nguvu zilizo timilifu, ijapokuwa ni wengi, hata hivyo watakatwa, naye atapita na kwenda zake. Ingawa nimekutesa, sitakutesa tena.

13. Na sasa nitakuvunjia nira yake, nami nitakupasulia mafungo yako.

14. Tena BWANA ametoa amri katika habari zako, ya kwamba asipandwe tena mtu awaye yote mwenye jina lako; toka nyumba ya miungu yako nitakatilia mbali sanamu ya kuchora, na sanamu ya kuyeyusha; nitakufanyia kaburi lako; kwa maana u mbovu.

15. Tazama, juu ya milima iko miguu yake aletaye habari njema, atangazaye amani. Zishike sikukuu zako, Ee Yuda, uziondoe nadhiri zako; kwa maana yule asiyefaa kitu hatapita kati yako tena kamwe; amekwisha kukatiliwa mbali.

Nah. 1