1. Na Mungu akamkumbuka Nuhu, na kila kilicho hai, na wanyama wote waliokuwamo pamoja naye katika safina; Mungu akavumisha upepo juu ya nchi, maji yakapungua;
2. chemchemi za vilindi zikafungwa, pia na madirisha ya mbinguni, mvua kutoka mbinguni ikazuiliwa;
3. maji yakadumu kuondoka katika nchi; na mwisho wa siku mia na hamsini maji yakapunguka.
4. Mwezi wa saba, siku ya kumi na saba ya mwezi, safina ikatua juu ya milima ya Ararati.
5. Maji yakapunguka-punguka hata mwezi wa kumi; mwezi huo wa kumi, siku ya kwanza ya mwezi, vilele vya milima vikaonekana.
6. Ikawa baada ya siku arobaini, Nuhu akalifungua dirisha la safina, alilolifanya;
7. akatoa kunguru, naye akatoka akaenda huko na huko, hata maji yakakauka juu ya nchi.
8. Kisha akatoa njiwa, aone kwamba maji yamepunguka usoni pa nchi;
9. bali yule njiwa hakuona mahali pa kutua kwa wayo wa mguu wake, akamrudia Nuhu safinani, maana maji yalikuwa juu ya uso wa nchi yote; naye akanyosha mkono, akamtwaa, akamwingiza mle safinani.
10. Akangoja na siku saba tena; kisha akamtoa yule njiwa katika safina mara ya pili,