Mwa. 5:7-11 Swahili Union Version (SUV)

7. Sethi akaishi baada ya kumzaa Enoshi miaka mia nane na saba, akazaa wana, waume na wake.

8. Siku zote za Sethi ni miaka mia kenda na kumi na miwili, akafa.

9. Enoshi akaishi miaka tisini, akamzaa Kenani.

10. Enoshi akaishi baada ya kumzaa Kenani miaka mia nane na kumi na mitano, akazaa wana, waume na wake.

11. Siku zote za Enoshi ni miaka mia kenda na mitano, akafa.

Mwa. 5