Mwa. 5:11-24 Swahili Union Version (SUV)

11. Siku zote za Enoshi ni miaka mia kenda na mitano, akafa.

12. Kenani akaishi miaka sabini, akamzaa Mahalaleli.

13. Kenani akaishi baada ya kumzaa Mahalaleli miaka mia nane na arobaini, akazaa wana, waume na wake.

14. Siku zote za Kenani ni miaka mia kenda na kumi, akafa.

15. Mahalaleli akaishi miaka sitini na mitano, akamzaa Yaredi.

16. Mahalaleli akaishi baada ya kumzaa Yaredi miaka mia nane na thelathini, akazaa wana, waume na wake.

17. Siku zote za Mahalaleli ni miaka mia nane na tisini na mitano, akafa.

18. Yaredi akaishi miaka mia na sitini na miwili, akamzaa Henoko.

19. Yaredi akaishi baada ya kumzaa Henoko miaka mia nane, akazaa wana, waume na wake.

20. Siku zote za Yaredi ni miaka mia kenda na sitini na miwili, akafa.

21. Henoko akaishi miaka sitini na mitano, akamzaa Methusela.

22. Henoko akaenda pamoja na Mungu baada ya kumzaa Methusela miaka mia tatu, akazaa wana, waume na wake.

23. Siku zote za Henoko ni miaka mia tatu na sitini na mitano.

24. Henoko akaenda pamoja na Mungu, naye akatoweka, maana Mungu alimtwaa.

Mwa. 5