Mwa. 5:1-8 Swahili Union Version (SUV)

1. Hiki ndicho kitabu cha vizazi vya Adamu. Siku ile Mungu alipoumba mtu, kwa sura ya Mungu alimfanya;

2. mwanamume na mwanamke aliwaumba, akawabariki akawaita jina lao Adamu, siku ile walipoumbwa.

3. Adamu akaishi miaka mia na thelathini, akazaa mwana kwa sura yake, kwa mfano wake, akamwita jina lake Sethi.

4. Siku za Adamu baada ya kumzaa Sethi zilikuwa miaka mia nane, akazaa wana, waume na wake.

5. Siku zote za Adamu alizoishi ni miaka mia kenda na thelathini, naye akafa.

6. Sethi akaishi miaka mia na mitano, akamzaa Enoshi.

7. Sethi akaishi baada ya kumzaa Enoshi miaka mia nane na saba, akazaa wana, waume na wake.

8. Siku zote za Sethi ni miaka mia kenda na kumi na miwili, akafa.

Mwa. 5