1. Yakobo akawaita wanawe, akasema, Kusanyikeni, ili niwaambie yatakayowapata siku za mwisho.
2. Kusanyikeni, msikie, enyi wana wa Yakobo,Msikilizeni Israeli, baba yenu.
3. Reubeni, u mzaliwa wangu wa kwanza,Nguvu zangu, na malimbuko ya uwezo wangu.Umewapita wengine kwa ukuu na kwa nguvu.
4. Umeruka mpaka kama maji, basi usiwe na ukuu,Kwa sababu ulikipanda kitanda cha baba yako,Ukakitia unajisi; alikipandia kitanda changu.